Kwa mujibu wa timu ya tarjama ya Shirika la Habari la "Hawza", Hojjat al-Islam wal-Muslimin Sheikh Ali Yassin, Mkuu wa Jumuiya ya Wanazuoni wa Tiro na vitongoji vyake, katika khutba yake ya Swala ya Ijumaa iliyofanyika katika Shule ya Kidini ya Tiro, huku akisisitiza haja ya kuambatana (na kushikamana) na Mamlaka na Umoja wa Lebanon katika hali inayotishia katika eneo la kikanda, amekumbushia akisema kwamba: Mpango wa Wazayuni na Wamarekani wa kutaka kuuacha mtupu ukanda wa Gaza kwa kuwahamsha wakazi wake, umechukuliwa ili kuigawanya Syria na vile vile kuidhoofika Lebanon kwa ajili ya kuutumikia utawala haram wa Israel unaoikalia kwa mabavu Palestina.
Suala hili liliibuliwa baada ya utawala huu haram kushindwa kufikia malengo yake licha ya kusababisha uharibifu mkubwa na kuwaua shahidi Wapalestina wengi.
Mwishoni, Khatibu huyu wa Lebanon alisema: Mpango wa Marekani wa kuuacha wazi Ukanda wa Gaza na kuwahamisha wakaazi wake hadi nchi jirani ni jaribio la kuunda janga jipya. Hatupaswi kujisalimisha kwa mradi wa Kizayuni-Kimarekani; Mradi unaotaka kuufanya utawala haram wa Israel kuwa Polisi wa eneo la kikanda ili kujihakikishia maslahi yake; na faida zinazogharimu kupoteza utu, usalama na maisha ya mataifa.
Your Comment