Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hazrat Ayatollah Nouri Hamedani, katika kikao na Mhandisi Mohammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran alisisitiza haja ya kudumisha nguvu na utayarifu dhidi ya maadui na kubainisha kuwa: Uislamu umekuwa ukizungumza juu ya nguvu (na heshima) na katika Kitabu cha Wasail al-Shia, mlango wa Jihad, hadithi ya kwanza toka kwa Imam Jafar Sadiq (a.s) amesema:
«الخَیرُ کُلُّهُ فی السَّیفِ وتَحتَ ظِلِّ السَّیفِ، ولا یُقِیمُ الناسَ إلاّ السَّیفُ، والسُّیُوفُ مَقالِیدُ الجَنَّةِ والنارِ»
Kheri yote ipo katika Jihad na chini ya kivuli cha Jihad, na hakuna (namna nyingine kwa watu) ispokuwa kufanya Jihad, na Jihad; ni funguo za pepo na moto – akasema: Kwa kuzingatia nafasi ya Mujahidina na suala la Jihad na nguvu (kumiliki uwezo wa kijeshi) na kusimama imara mbele ya maadui, kuwa ni jambo muhimu sana, na kwa mantiki hiyo kazi yenu na juhudi zenu katika uwanja huu zitakuwa ni muhimu sana na ni za lazima.
Katika Hadithi hii, makusudio ya Hazrat Imam Saduq (a.s) kuhusu Jihad ni kuwa na nguvu (za kijeshi) na maandalizi (ya kutosha) dhidi ya maadui.
Hadhrat Ayatollah Al-Udhma Nouri Hamedani amepongeza juhudi za vijana na wanasayansi wenye dhamira ya dhati katika maendeleo na mafanikio ya nchi katika mjadala wa sekta ya nyuklia na kuongeza kuwa: Tunaona kuwa ujenzi wa bomu la nyuklia ni Haram, lakini tunaona kuwa ni nyeti na ni muhimu kujilinda dhidi ya maadui na kufanya jambo lolote linalochangia maendeleo ya nchi na faraja na ustawi wa wananchi.
Akirejelea ahadi mbovu ya Marekani, amekumbushia akisema: Marekani ni adui yetu na hatuna shaka na suala hili, na hata leo hii utawala haram wa mauaji ya watoto wa Israel unafanya jinai chini ya kivuli cha Marekani. Ikumbukwe kwamba mazungumzo yoyote yanapaswa kutoka kwenye nafasi ya nguvu na heshima ya watu; Kwa bahati mbaya, wengine husema na kuongea maneno kwa udhaifu. Hatupaswi kujionyesha kuwa sisi ni dhaifu mbele ya adui na tunakiwa kusimama imara dhidi ya njama zao kwa umoja wetu na tuonyeshe heshima na (uwezo) nguvu zetu.
Your Comment