Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hojjatul-Islam wa al-Muslimeen Syed Mufid Hosseini Kohsari, katika mpango wa kwanza wa mfululizo wa programu za Kimataifa za Msikiti Mtakatifu wa Jamkaran katika Mnasaba wa nusu ya Sha'ban, ambao ulifanyika mbele ya Mashia wanaozungumza Kimalaysia kutoka Indonesia, Malaysia, Thailand na Kambodia katika eneo la Msikiti Mtukufu wa Jamkaran, na akiashiria katika baadhi ya Aya za Qur'an Tukufu alisema: Sura saba zinazoanza kwa Kumsabihi Mwenyezi Mungu zinaitwa "Surah Musabahat" na katika riwaya tunayo kauli hii kwamba yeyote ambaye anatafuta ukaribu na Sura hizi saba atakuwa anatafuta ukaribu na Imam wa Zama (a.s).
Akiashiria kwamba surah hizi zinatukuza na kutakasa na zinaweza kumtakasa mtu binafsi, jamii na ulimwengu kwa ujumla, alieleza akisema: Tumeelekezwa katika Hadithi kwamba tunapaswa kuwa na matarajio ya vitendo na yenye ufanisi wakati wa ghaiba na Mtiririko wa Haki unapaswa kujitayarisha wenyewe kwa ajili ya matukio ya kudhihiri.
Makamu wa Rais wa mawasiliano na masuala ya kimataifa wa seminari (Hawza) alifafanua baadhi ya mikakati iliyowasilishwa katika “Surah Musabahat” na akasema: Mkakati wa Surah al_Jumuah ni huu kwamba tuwe na mkusanyiko wa kusubiri faraja, na Sala ya Ijumaa ni alama ya mkusanyiko wa Waumini na Umoja wa Waumini.
Hosseini Kohsari aliongeza: Jambo muhimu zaidi la Surat al_Saf ni hili kwamba lazima tupigane dhidi ya maadui, ambapo hilo ni mfano wa wazi wa Mapambano ya Upinzani (Muqawamah) katika eneo la kikanda.
Aliendelea: Katika Surat al_Hadid, Mwenyezi Mungu pia anasisitiza uadilifu, na ikiwa sisi tunatafuta kuyafikia maisha ya Mahdawi (Imam Mahdi), basi ni lazima tufanye Harakati kwa kupitia katika Njia ya Uadilifu.
Makamu wa rais wa mawasiliano na masuala ya kimataifa ya Seminari (Hawza) alibainisha kwamba katika riwaya imeashiriwa kwamba, Bendera moja na Serikali moja itaundwa katika ardhi ya Uajemi katika zama za mwisho, na baada ya hapo Sayansi na Maarifa ya Ahlul-Bayt (a.s) vitaenea kwa ulimwengu wote, alibainisha akisema: Katika riwaya imesisitizwa kuwa, Wazayuni wataangamizwa kupitia Mapinduzi hayo, na Waislamu na Wapenzi wa Ahlul-Bayt (a.s) watakuwa na izza na utukufu, na Serikali hii itakuwa msingi wa Hadhrat al_Hojjat (a.t.f.s).
Your Comment