Kwa mujibu wa Shirika la habari la Hawza, Hayati Ayatollah Mohammad Ali Naseri, mmoja wa maprofesa wa maadili wa Hawza, katika moja ya masomo yake ya maadili juu ya mada ya "Hofu na Matumaini; ni mabawa mawili ya kuruka kuelekea kwa Mwenyezi Mungu" ambapo andiko lake ni kama ifuatavyo:
Hofu na kuwa na matumaini ni sifa tofauti za watu Wacha Mungu na Mawalii wa Mwenyezi Mungu. Imeelezwa katika Hadithi kwamba hofu na matumaini ya waumini yanapaswa kusawazishwa sawa na ncha mbili za mizani, lakini katika baadhi ya hadithi imesisitizwa kwamba matumaini zaidi ni bora zaidi.
Hofu imegawanywa katika aina mbili: "Hofu ya kulaumiwa" na "Hofu ya kusifiwa".
Kutenda dhambi ni kukosa aibu kubwa:
Hofu ya kusifiwa, ni kama (kuwa na hofu au) kuogopa adhama na ukuu wa Mwenyezi Mungu, kuogopa haki na uadilifu wa kimungu, au mtu kuogopa matendo yake binafsi. Kwa mfano, mtu ambaye amefanya uhaini na ni lazima aende mahakamani, ni kawaida kuwa na hofu.
Kwa hakika, «الخائنُ خائفٌ» (msaliti - mhaini, mfanya khiana - huwa anaogopa na kuwa na hofu). Sisi sote ni wasaliti kwa Mwenyezi Mungu na moja ya mifano ya usaliti huu ni dhambi zetu.
Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an: Matendo yako na tabia yako viko chini ya udhibiti. Malaika wawili wanaoitwa "Raqib" na "Ateed" ni mashahidi na wanaangalia matendo yetu.
Katika uwepo wa Mwanadamu, kuna akili na nafsi, ambapo kila moja wapo ina jeshi lake na kila wakati kuna migogoro kati yao. Ikiwa akili itaishinda (nafsi), basi Mwanadamu huyo atafikia nafasi ya kuwa na ukaribu na Mwenyezi Mungu; Vinginevyo (ikiwa akili itashindwa na nafsi na nafsi ikatawa akili yake), basi kwa hakika nafsi itapata tabu na itatumbukia kwenye ufisadi mkubwa.
Hofu juu ya matendo mabaya ni hofu iliyokuwa nzuri, kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa matendo yetu. Imeelezwa katika Qur'an Tukufu:
«وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَیۡهِ مِنۡ حَبۡلِ ٱلۡوَرِیدِ»
(Tuko karibu naye zaidi kuliko mshipa wa shingo yake) na pia:
«هوَ مَعَکُمْ أَیْنَ ما کُنْتُمْ»
(Yuko pamoja nanyi popote mlipo).
Hata hivyo, ni aibu kubwa kufanya dhambi (na maasi). Maasumina (14), Malaika, Ardhi, Mchana na Usiku na hata viungo vya miili yetu, wanashuhudia matendo yetu, na watashuhudia Siku ya Kiyama.
Ikiwa tunaogopa ushuhuda huu, hii itakuwa ni hofu nzuri. Ili kuepushwa na matokeo ya matendo (yetu), ni lazima tutubu; na iwe ni Toba ambayo inaambatana na majuto kwa yaliyopita na uamuzi wa kuacha dhambi siku zijazo. Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa Kurehemu na ni Mwingi wa kusamehe.
Kumcha Mwenyezi Mungu humwokoa mtu asitumbukie katika shimo la dhambi
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Mimi namuogopa Mwenyezi Mungu kuliko nyinyi nyote." Imamu Sajjad (amani iwe juu yake) alikuwa akitetemeka kwa kuogopa adhama na ukuu wa Mwenyezi Mungu wakati wa swala yake.
Imamu Sadiq (amani iwe juu yake) naye alikitetemeka sana kutokana na kuwa na khofu ya Mwenyezi Mungu na pale alipovaa Ihram kwa ajili ya Ibada ya Hijja hakuwa akiweza hata hakusema (talbiyah) ya "Labbaika" - kutokana na wingi wa hofu aliyokuwa nayo juu ya adhama na ukuu wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) -.
Walipomuuliza: Kwa nini husemi Talbiyah? Akasema: "Nachelea kusema "Labbaika Allahumma, Labbaika" na Mwenyezi Mungu ajibu: Hapana La Labbaika na wala La Saadaika."
Imepokewa pia kwamba Imamu Sajjad (amani iwe juu yake) alikuwa anaswali, wakati huo mmoja wa watoto wake alitumbukia kwenye kisima. Watu waliokuwa karibu walimuokoa mtoto wake, lakini Imamu hakutambua hili mpaka mwisho wa swala yake.
Walipomuuliza: Je, hukutambua? Akasema: "Nilitikiswa sana na ukuu wa Mwenyezi Mungu kiasi kwamba hata sikuelewa / sikutambua." Hofu hii ya ukuu na uadilifu wa Mwenyezi Mungu ni woga mzuri (au ni hofu iliyokuwa nzuri) na ni ishara ya imani.
Amirul Muminin (amani iwe juu yake) anasema:
«الخَوفُ سِجْنُ النّفْسِ عَن الذُّنوبِ ورادِعُها عنِ المَعاصی»
(Kumcha Mwenyezi Mungu huifungia nafsi kutokana na dhambi na kuizuia na maasi).
Ikiwa unamcha Mwenyezi Mungu, hofu hii ni kama gereza linalokuzuia usitende dhambi na kukutawala. Hofu hii humuokoa mtu asitumbukie katika shimo la dhambi na kufungua njia ya kuifikia rehema ya Mwenyezi Mungu isiyo na kikomo.
Your Comment