Kwa mujibu wa Shirika la habari la Hawza, Hadhrat Ayatollah Shabiri Zanjani katika ujumbe wake wa Maandishi, huku akitoa pongezi kwa kuwasili kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Mwezi wa Elimu, Ibada na Huduma, Mwezi wa kuteremshwa Qur'an ndani yake, na sikukuu isiyo na kikomo ya Mwenyezi Mungu, amezungumzia juu ya umuhimu wa Mwezi huu na kusema:
Hadhrat Imamu Sadiq (amani iwe juu yake) amesema:
Mwezi wa Ramadhani pndi uluokuwa mpya (kwa kuandama), Hadhrat Amirul-Mu'minan (amani iwe juu yake), alikuwa akielekea Kibla na kisha anaomba dua hii namna hii:
«اللَّهُمَّ أَهِلَّهُ عَلَیْنَا بِالْأَمْنِ وَالْإِیمَانِ وَالسَّلَامَةِ وَالْإِسْلَامِ وَالْعَافِیَةِ الْمُجَلِّلَةِ، اللَّهُمَّ ارْزُقْنَا صِیَامَهُ وَقِیَامَهُ وَتِلَاوَةَ الْقُرْآنِ فِیهِ، اللَّهُمَّ سَلِّمْهُ لَنَا وَتَسَلَّمْهُ مِنَّا وَسَلِّمْنَا فِیه.»
Eee Mwenyezi Mungu! Ufanye Mwezi huu kuwa mpya kwetu kwa usalama, imani, afya, Uislamu na siha njema.
Eee Mwenyezi Mungu! Turuzuku kuufunga Mwezi huu, kukesha usiku wake, kuabudu, na kusoma Qur'an ndani yake.
Eee Mwenyezi Mungu! Ujaalie Mwezi huu wa Ramadhani uwe na afya njema (na salama) kwa ajili yetu, na uupokee kutoka kwetu ukiwa salama, na utujaalie swiha na afya njema katika Mwezi huu.
Al-Kafi: Juzuu ya 4. Ukurasa wa 73. Hadithi 4.
Your Comment