Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Samahat Sheikh Miraj Salim, amebainisha kuwa Mwezi Mtukudu wa Ramadhan ni Mwezi katika Miezi Kumi na Miwili ya Mwenyezi Mungu. Lakini Mwezi huu unasifa za kipekee tofauti na Miezi mingine, na hiini kwa sababu Mwenyezi Mungu ameubariki sana. Na ndio maana, pindi unapoingia Mwezi huu, Dunia nzima inauzungumzia, na kuupa heshima kubwa sana.Waislamu wanauheshimu Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, na hata wasiokuwa Waislamu pia wanauheshimu.
Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) anasema kuwa: Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan umetujia ukiwa na Sifa Kuu Tatu:
Umetujia kwa Baraka za Mwenyezi Mungu, Huruma ya Mwenyezi Mungu , Na Maghfira na Msamaha wa Mwenyezi Mungu (swt). Hivyo Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan ni Mwezi wa Baraka, ni Mwezi wa Rehma, na ni Mwezi wa Maghfira.
Lakini Una Sifa nyingine kuu, nayo ni: Kuwa Mwezi huu ni bora zaidi kuliko Miezi mingine. Na Masiku yake ni Masiku Bora kuliko Masiku Mengine.
Your Comment