Thursday 20 February 2025 - 13:32
Hakuna mtu ana haki ya kuharibu utu (heshima) yake

Hawzah/ Hadhrat Ayatollah Jawadi A'mouli amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi sifa (heshima) ya Muumini na akasema: Heshima ya Muumini ni amana ya Mwenyezi Mungu. Heshima yake ni ya Mwenyezi Mungu, kwa hiyo hakuna aliye na haki ya kudhuru heshima yake.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mkutano wa kila wiki wa somo la maadili (Akhlaq) la Ayatollah Jawadi A'mouli ulifanyika leo (Jumatano) katika Msikiti Mkuu wa Qom kwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Katika mkutano huu, Hadhrat Ayatollah Jawadi A'mouli alielezea hekima ya 159, 160 na 161 ya Nahj al-Balaghah na akasema: Hadhrat Amirul Momineen (AS) anasema katika khutba ya 159 ya Nahj al-Balaghah:

«مَنْ وَضَعَ نَفْسَهُ مَوَاضِعَ التُّهَمَةِ، فَلَا یَلُومَنَّ مَنْ أَسَاءَ بِهِ الظَّنَّ»

Kwa maana kwamba: Mtu anayejianika kwa uchongezi dhidi ya Nafsi yake (au anayejiweka mwenyewe katika Nafasi ya kutuhumiwa), huyo hapaswi kuwalaumu watu wengine kwa kumshuku (na kumtuhumu).

Alisema: Kuwa katika hali zenye kutiliwa shaka na mahali pa kukashifiwa ni jambo lisilofaa kidini na kunaweza kudhuru (heshima na) utu wa mtu. Kama Amirul Momineen (AS) alivyosema, kama mtu atajiweka wazi kwa kashfa, huyo hatakiwi kulalamika kuhusu tuhuma za wengine juu yake.

Hadhrat Ayatullah Jawadi A'mouli alisisitiza umuhimu wa kuhifadhi Heshima ya Muumini na akasema:

Heshima ya Muumini ni amana ya Mwenyezi Mungu; Mwanadamu ndiye mwenye mali anayochuma, lakini Heshima yake ni ya Mwenyezi Mungu. Heshima ya Muumini hupatikana kwa sababu ya imani yake na inachukuliwa kuwa amana ya kimungu. Kwa hiyo, hakuna mwenye haki ya kudhuru Heshima yake, kama vile jamii ya Kiislamu isijidhihirishe kuwa dhalili na isijiweke kwenye Hali ya kudhalilishwa.

Akirejelea Hadithi kutoka ndani ya Usul al_Kafi, alifafanua: Mwenyezi Mungu (SWT) alikabidhi mambo yote ya Muumini kwa nafsi yake, lakini hakumuachia Muumini mwenyewe kulinda utu na heshima yake, kwa sababu heshima ni ya Mwenyezi Mungu, kama ilivyoelezwa katika Qur'an Tukufu:

﴿العِزَّةُ لِلَّهِ جَمِیعًا﴾

"Heshima yote (Utukufu wote) ni wa Mwenyezi Mungu".

Kwa hiyo, Muumini ni mtunza Amana ya Mwenyezi Mungu katika kulinda Heshima yake na hapaswi kufanya jambo lolote linaloharibu heshima yake ya kidini.

Hadhrat Ayatollah Jawadi A'mouli aliendelea kueleza hekima ya 160 na akasema: Hazrat Ali (a.s) anasema:

"منْ ملكَ اسْتأثَرَ"

Kwa maana kwamba: Yule ambaye anakuwa mmiliki huwa anataka kuhodhi (anakuwa na ukiritimba).

Akifafanua hili, alisisitiza kuwa ukiritimba huu unaweza kuonekana katika nyanja za kifedha, kisiasa na kijamii.

Mheshimiwa alisema: Mtu akipata mtaji, anajaribu kuongeza kiasi chake, na akipata mamlaka(hivyo hivyo), anajaribu kulazimisha utawala wake na kuwaweka wengine chini ya udhibiti wake. Tamaa hii ya ukiritimba imesababisha dhuluma mara nyingi katika historia (ya Mwanadamu).

Akaongeza: Baadhi ya wafasiri wamelifasiri neno "istiithar" kuwa lina maana ya dhulma na wamezingatia neno “Kumiliki” sio neno linalotoka kwenye mzizi wa wa Neno “Mmiliki / Ma'lik” bali linatoka kwenye neno “Maluk / Wafalme ”, lakini katika hali zote mbili maana kuu ya sentensi hii ni kusisitiza hatari ya kuhodhi madaraka na mali.

Hadhrat Ayatollah Jawadi A'mouli alirejea tena kwenye Hekima ya 161, ambayo Amirul Momineen (AS) anasema:

« مَنِ اسْتَبَدَّ بِرَأْیِهِ هَلَكَ، وَ مَنْ شَاوَرَ الرِّجَالَ شَارَکَهَا فِی عُقُولِهَا»

Kwa maana: Anayetegemea maoni (rai) yake tu ataangamia. Ubabe, kujiona kuwa mwadilifu na kutozingatia mashauriano (mabadilishano ya Fikra, Rai na Maoni) hupelekea uharibifu wa mtu binafsi na jamii.

Kisha Mheshimiwa akaendelea kueleza nafasi ya akili katika mfumo wa elimu ya Uislamu na, akinukuu maneno ya Amirul-Mu’minin (amani iwe juu yake), katika Nahj al-Balagha, ambapo alieleza kuwa akili ni sababu ya kupambanua haki na batili na ni kipimo cha kupima matendo ya Mwanadamu.

Akiashiria uhusiano uliopo kati ya Akili ya kinadharia na Akili ya Kimatendo, alikazia akisema:

Furaha ya Mwanadamu inategemea matumizi sahihi ya akili yake na kuepuka ubinafsi. Akili humuepusha Mwanadamu na Ujinga na Upotofu na humuongoza kuelekea kwenye njia iliyo sawa (iliyonyooka).

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha