Friday 7 February 2025 - 06:32
Uzalishaji wa mawazo sehemu muhimu ya shughuli za Seminari (Hawza)

Mkuu wa Jumuiya ya Walimu wa Seminari (Hawza) ya Qom alisisitiza juu ya haja ya uwepo wa utafiti wa kimfumo katika seminari na akasema: “Uzalishaji wa mawazo ni sehemu muhimu ya shughuli za seminari(Hawza)”. Lau Sheikh Ansari angekuwa miongoni mwetu leo hii, angeandika kazi zake kwa kuzingatia mahitaji ya siku ya leo (zama za leo) na matarajio ya dunia ya sasa, na hii ni kwa vile mazingatio yake pia yalitolewa kwa kulingana na mahitaji ya wakati huo.”

Shirika la Habari la Hawza - Mkuu wa Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom Ayatollah Sayyid Hashem Hosseini Bushehri alitoa hotuba katika hafla ya kuhitimisha toleo la 26 la Kitabu cha Mwaka wa Seminari katika Seminari ya Imam Kadhim (a.s) huko katika Mji wa Qom, akisema: "Ayatollah Al-Udhma Shobeiri Zanjani anazingatiwa kuwa miongoni mwa waanzilishi wa enzi za sasa, na alithaminiwa (na kutunukiwa na kupewa heshima yake) katika kongamano hili."

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu amebainisha zaidi kuwa Hayati Ayatollah Rey Shahri pia alifanya juhudi za ikhlasi kwa miaka mingi katika nyanja mbalimbali hususan katika uga wa Hadithi ambapo pia alitunukiwa na kuthaminiwa katika kongamano hili.

Mkuu wa Jumuiya ya Walimu wa Seminari ya Qom aliendelea kwa kusema kuwa: “Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliichukulia kalamu kuwa ni baraka kubwa iliyopelekea maendeleo ya Dini, Dunia na Maisha (ya Mwanadamu).

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha