Tuesday 4 March 2025 - 15:18
Programu za huduma na utamaduni wa Madhabahu (Haram) Tukufu ya Hazrat Abbas (AS) wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Hazwa / Madhabahu Tukufu ya Hazrat Abbas (amani iwe juu yake), imepitisha programu kadhaa za huduma na kitamaduni za kuwapatia Mazuwwari katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kwa mujibu wa kundi la Tarjama la Shirika la Habari la Hawza, programu za Hadhrat Abbas (amani iwe juu yake), ambazo ni pamoja na kuhitimisha kisomo cha Qur'an, usomaji wa Qur'an kwa utaratibu (Tartil), na ufundishaji wa Qur'an, na mihadhara ya kidini ya kila siku.

Kufanyika kwa shindano la pili la kimataifa la Tuzo la "Al-Amid" kwa ajili ya kusoma Qur'an Tukufu pia ni moja ya programu muhimu za Madhabahu Tukufu ya Hazrat Abbas (amani iwe juu yake).

Madhabahu (Haram) hii Tukufu ina programu maalum za ibada kwa mikesha yenye baraka ya Lailatul- Qadr na hafla zingine za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Redio ya Wanawake ya Al-Kafil, inayoshirikiana na idara ya masuala ya kiakili ya Haram hii Tukufu, pia itatayarisha na kutangaza vipindi kadhaa maalum vya redio kwa Mwezi huu Mtukufu.

Wakati wa Mwezi Mtukufu, milo ya iftar na daku imeandaliwa kwa watu wanaofunga (Mwezi Mtukufu wa Ramadhan). Mabasi pia yameandaliwa ili kuwasafirisha Mazuwwari wakati wa siku za msongamano wa watu katika Madhabahu (Haram) ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha