Monday 3 March 2025 - 23:02
Tuwapende na Kuwakirimu Mayatima

Hawza / Uislamu umetuelekeza na kutuhimiza kuwapenda, kuwakirimu na kuwahurumia Mayatima, na kutokuwaonea.

Shirika la Habari la Hawza, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo hii leo tarehe 3 Machi, 2025, ameandaa hafla kubwa ya kuwafuturisha Watoto Yatima na Watoto wenye Mahitaji Maalum, katika Viwanja vya Ikulu, Jijini Dar -es- Salaam,Tanzania.

Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewaasa Waislamu na Wageni wote waalikwa katika hafla hiyo juu ya kuwapenda, kuwakirimu na kuwahurumia Mayatima na kutokuwaonea, akisema kuwa hilo ndio Agizo Tukufu la Mwenyezi Mungu pale aliposema:

﴿فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ

"Basi Yatima Usimuonee" [Surah Dhuha: Aya ya 9].

Aidha, ametumia fursa hiyo kuwaasa Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla kuwa na desturi ya kuwajali na kuwakirimu kwa wingi Masikini, watu wasiojiweza na Watoto Yatima hususan katika Mwezi kama huu Mtukufu wa Ramadhan, na kwamba hilo ndio jambo zuri na jema analolipenda kuliona zaidi Mwenyezi Mungu katika jamii zetu kwamba tunahurumiana sisi kwa sisi na kukirimiana na kulishana chakula kizuri, hasa chakula kile kinachopendwa zaidi na nafsi zetu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t):

﴿وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا

"Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, Masikini, na Yatima, na Wafungwa".[Surah Al-Nisaa: Aya ya 8].

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha