Monday 3 March 2025 - 22:57
Chochote unachokijua kuwa hiki kina kheri, basi usiache kupambana kukifanya

Hawza / Kumswalia Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) kwa wingi ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuna kheri nyingi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Walid Al-Hadi, ambaye ndiye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salam, Tanzania, Chini ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), na Imam Mkuu wa Masjid Kichangani, Dar-es-Salam, amesisitiza kwa Waumini wa Kiislamu katika Darsa lake la Mwezi Mtukufu wa Ramadhan linalofanyika kila siku ndani ya Masjid Kichangani kuwa ni muhimu kwako Muumini: Chochote kile unachokijua kuwa hiki kina Kheri ndani yake, basi usiache kupambana kukifanya.

Akifafanua na kubainisha nukta hiyo, ameashiria baadhi ya mifano ya mambo kadhaa yenye kheri nyingi ndani yake, akisema: Kwa mfano: Kumswalia Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) kwa wingi ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuna kheri nyingi, vile kutoa Sadaka, kufanya ibada mbalimbali, kuhudhuria katika Darsa za kujifunza Qur'an Tukufu na masomo mbalimbali ya Dini Tukufu ya Kislamu, n.k. Kuwa na Nia nzuri katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ya kufanya mambo ya kheri na Kumtii Mwenyezi Mungu ili uchume thawabu nyingi.

Aidha, amewakumbusha Waumini kuhusiana na nasaha ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) kuwa ametusisitiza sana kuomba kwa wingi vitu vitatu ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, navyo ni hivi vifuatavyo:

1_Usiache katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan kulitaja sana neno "Astaghfirullah".

2_Kithirisha sana kuomba Pepo.

3_Kithirisha sana kumuomba Mwenyezi Mungu akuepushe na Moto wa Jahannam, hasa baada ya Swala yako, usisahau kuomba hilo.

Ukifanikiwa katika hayo matatu, umefaulu Duniani na Akhera.

Na kwanini tunasema kuwa uombe zaidi baada ya Swala? Kwa hakika ni kwa sababu baada ya Swala ni wakati muhimu mno ambao Allah (s.w.t) anasikiliza sana na kujibu kwa wingi Dua za waja Wake.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha