Monday 3 March 2025 - 10:17
Ramadhani ni wakati wa utakaso wa nyoyo

Hawza / Hazrat Ayatollah Javadi Amoli amefafanua: Moyo sio kama dimbwi ambalo maji yake yanaweza kusafishwa kwa urahisi, au kama mkondo na vijito vidogo ambavyo ni rahisi kusafisha [badala yake] - Moyo - unahitaji chombo chenye nguvu cha kuutakasa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hazrat Ayatollah Javadi Amoli, akizungumzia kuwasili kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, amezungumzia juu ya maudhui ya "Utakaso wa Moyo, ni njia ya kujibiwa maombi (dua)" na kusema: “Mwezi huu (Ramadhan) pia ni Mwezi ambao mtu akitaka kujibiwa maombi (dua) yake kwanza ajitakase na kutafuta jawabu la maombi yake (kuanzia) ndani ya nafsi yake, na nafsi (roho) yetu pia ni bahari, si kama sisi ni msururu tu wa sayansi ya upatikanaji, mawazo na uthibitisho na tuwe na mipaka kwa haya. Sio sahihi kwamba tutafute msururu huu mrefu wa Sayansi za kutafuta (na kuchuma), za kufikiri na kusadikisha, kisha tuwe ni watu wa muhtasari katika hayo.

Katika Majlis ya 7 ya Amali, ya Marehemu Sheikh Mufid (radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), Hadithi ya kwanza ni hii kwamba, imepokewa kutoka kwa Imamu Sadiq (rehema na amani ziwe juu yake), kuwa amesema:

«تَبَحَّرُوا قُلُوبَكُمْ فَإِنْ أَنْقَاهَا اَللَّهُ مِنْ حَرَكَةِ اَلْوَاجِسِ لِسَخَطِ شَيْءٍ مِنْ صُنْعِهِ فَإِذَا وَجَدْتُمُوهَا كَذَلِكَ فَاسْأَلُوهُ مَا شِئْتُمْ

Jitakaseni (nafsi / nyozo zenu), kwa ufupi ni kwamba, Moyo huu si kama dimbwi ambalo maji yake yanaweza kusafishwa kwa urahisi au kama mkondo na vijito vidogo ambavyo ni rahisi kusafisha [badala yake] - Moyo - unahitaji chombo chenye nguvu cha kuutakasa. Akasema: Safisheni bahari ya mioyo yenu, mtabahari (mzame zaidi) katika kuujua moyo... .

Somo la Tafsiri ya Surah Al-Imran: Kikao cha 5.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha