Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Arafi, Mkurugenzi wa Seminari nchini (Iran), alitoa ujumbe kwa mnasaba wa mahudhurio yenye hamasa ya safu ya Upinzani (Muqawamah) kwenye Mazishi ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah, ambapo (Nakala) Maandiko yake ni kama ifuatavyo:
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
﴿یا أَیَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ ارْجِعِي إِلی رَبِّكِ راضِیَةً مَرْضِیَّةً فَادْخُلِي فِي عِبادِي وَ ادْخُلِي جَنَّتِي﴾
"Ewe nafsi iliyotua!, Rejea kwa Mola Wako hali ya kuwa radhi umeridhiwa" (Surat al_Fajr: Aya ya 27 - 28).
Ndugu Mabibi na Mabwana, Watoto wa Taifa kubwa la Lebanon na Watoto wa Imam Sayyid Musa Sadr, Sheikh Ragheb Harb, Sayyid Abbas Mousawi, Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiyyud-Din; (Amani, Rehema na Baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yenu).
Kwa kuuawa Shahidi Katibu Mkuu, Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah (Mwenyezi Amlaze Mahali Pema Peponi), leo Dunia yetu imempoteza Kiongozi ambaye pengi lake haitazibwa na chochote. Kama alivyosema Imamu Sadiq (amani iwe juu yake):
«إذا ماتَ المؤمنُ الفَقیهُ ثُلِمَ في الإسلامِ ثُلمَةٌ لا یَسُدُّها شيء».
«Muumini Faqih (Mwenye ilmu) wa anapofariki, ulimwengu wote wa Kiislamu unapata pengo ambalo hakuna kinachoweza kuliziba».
Maneno hayawezi kutosha kueleza masikitiko yetu kwa kumpoteza Sayyid wa Mashahidi wa Upinzani (Muqawamah) na Ndugu yake rafiki yake Mwaminifu, Sayyid Hashim Safiyyud_Din (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao). Viongozi hawa wawili waaminifu walipokea nishani ya heshima ya Kifo cha Kishahidi na leo hii "Wanafurahishwa na kile alichowapa Mwenyezi Mungu kutokana na Fadhila Zake, na wanafurahi kwa wale wanaowafuata (nyuma yao) ambao bado hawajajiunga nao, kwamba hakuna hofu juu yao na wala hakuna / hawana huzuni", Lakini maadui zao na wauaji wahalifu "Wanapaswa kucheka kidogo na kulia sana kwa sababu ya adhabu ya matendo waliyoyafanya (inayowangojea)", kwa sababu Ahadi ya Kisasi cha ki_Mungu ni ya kweli, kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t):
﴿إِنَّا مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنْتَقِمُونَ﴾
"Sisi tutalipiza Kisasi kwa Wahalifu (Waovu)". (Surat Sajdah: Aya ya 22).
Adui Mzayuni alifanya ijtihada za kumshinda Shahidi Nasrallah kwa kumuua kigaidi, lakini mafuriko ya machozi na nyoyo zilizojaa huzuni katika mazishi ya milioni ya watu, yalitoa pazia na kudhihirisha ukweli na uhakika ulioonyesha kwamba Damu yake Safi imeshinda Upanga.
Ushindi huu ulipatikana kwa hatua thabiti na azma ya wafuasi wa Faqih (Msomi) huyu Mwenye kupigana Jihad, na ukweli huu ni dalili ya kushindwa kwa maadui kufikia malengo yao.
Kuwepo (kuhudhuria kwa) mamilioni ya watu katika Mazishi ya Shahidi huyo mkubwa, ambayo yaliambatana na ushiriki wa watoto wa (Jamii zote na) makabila yote ya Lebanon baina ya Waislamu na Wakristo na Wafuasi wa mikondo tofauti ya Kisiasa, kuliimarisha Umoja wa Jamii ya Lebanon na kuthibitisha kwa mara nyingine tena kwamba Muqawamah ni ngao ya ulinzi wa ardhi hii na upanga wa Lebanon ambao unaweza kutegemewa kupigana dhidi ya uadui wa utawala ghasibu wa Kizayuni.
Pia uwepo wa ndugu wa Kisunni katika hafla hii ya mazishi uliashiria mafanikio ya juhudi za Shahidi huyu Sayyid katika kuimarisha Umoja na Mafungamano baina ya wafuasi wa Madhehebu za Kiislamu.
Ushiriki mkubwa na mshikamano wa Harakati ya Amal na Hezbollah katika Mazishi haya ulitoa pigo kwa wafitinishaji na kuwafahamisha ukweli na uhakika kwamba kamwe hawataweza kuleta fitna miongoni mwa wafuasi wa Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao), na kundi lenye sharafu la Mashia nchini Lebanon bado liko nyumbani; Na hii ina maana kwamba Bunge Kuu la Kiislamu la Shia (Nchini Lebanon) litaendelea kuwa na nguvu na utulivu.
Mazishi ya milioni ya watu, hafla ya kuheshimu na kuadhimisha na kufanya mazishi ya kiishara ya Shahidi huyo Mtakatifu katika nchi zingine, yaliyofanywa sambamba na hafla ya mazishi huko Lebanon, inaonyesha kwamba ujumbe wake umewafikia mataifa na watu huru wa ulimwengu wote. Mahudhurio haya ni ushahidi wa kuongezeka nguvu maarufu ya Hezbollah miongoni mwa mataifa ya eneo la kikanda na watu huru wa Dunia nzima, na kunaonyesha azma ya Harakati hii ya kuendelea kuwepo katika uwanja huo. Ukweli huu ndio utakaorudisha tena mlingano ya wa kutisha kwenye kina kirefu cha maeneo (ya Palestina) yanayokaliwa kimabavu (na Israel).
Seminari / Hawza zinasisitiza kwa mara nyingine tena kwamba Upinzani (Muqawamah) dhidi ya uvamizi (wa Kizayuni) ni wajibu wa kidini, na unatokana na imani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mafundisho ya Qur'an Tukufu na Sunnah Tukufu za Kinabii, na Seminari (Hawza) daima zimesimama kwenye mikondo na mienendo ya Upinzani (Muqawamah) na ndugu zao Mujahidina, na kwa hiyo, waliona kuwa ni wajibu wao kufanya kazi na wajumbe wa ngazi za juu na Maprofesa Mashuhuri ambao ni wawakilishi wa Marajii wa Kidini, na kuhudhuria katika mazishi haya na kutangaza kuunga mkono wajibu huu wa ki_Mungu. Vile vile wametoa salamu zao na shukrani zao kwa mikondo yote, shakhsia, koo, Wafuasi wa Dini na Madhehebu mbalimbali na watu huru wa Ulimwengu mzima walioshiriki katika Maombolezo haya ya Kitaifa, na wanatamani kwamba ushindi wa mwisho na kutoweka kwa uvimbe wa Saratani wa Uzayuni kutoka eneo hili la kikanda upatikane haraka iwezekanavyo.
﴿وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِنْدِ اللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ﴾
"Na hapana Nusra ila itokayo kwa Mwenyezi Mungu Matukufu, Mwenye Hekima". (Sarah Aali Imran: Aya ya 126).
Alireza Arafi
Mkurugenzi wa Seminari
Mji Mtakatifu wa Qom
Your Comment