Sunday 23 February 2025 - 08:03
Kumbukumbu za wasomi | Mfungwa ambaye aliwageuza wafungwa wa jela wa Kiyahudi na Wakristo kuwa Waislamu

Ayatollah Bafqi, kama Hadhrat Yusuf (a.s), aligeuza gereza zima kuwa Shule ya Tauhidi, kwa mahubiri (mawaidha) na ibada yake, aliwaongoa wafungwa na hata kuwasilimisha Maofisa wa Kiyahudi na Wakristo. Kwa Imani yake safi, alifungua nyoyo na kugeuza gereza la Pahlavi kuwa Msikiti.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika ripoti za Hayati Ayatollah Bafqi, imeelezwa kama ifuatavyo kuhusu Swala na Dua zake kwa Mwenyezi Mungu akiwa katika jela za Pahlavi (kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran) na namna alivyoleta mabadiliko kwa wafungwa:

Marehemu Ayatollah Bafqi aliipinga Serikali ya Pahlavi mara kadhaa hadi akafungwa jela.

Hata hivyo, hali ya jela ilibadilika mara moja kwa (wafungwa) wote kutokana na vilio, maombolezo, swala na dua za mtu huyu mkubwa na kugeuka kuwa Msikiti.

Idadi kubwa ya wafungwa waliongoka (na Kutubu) na wakawa wakiswali swala za Jamaa Mwanzo wa wakati wakiwa chini ya Uimam wake.

Baada ya mawaidha yake, kama ilivyokuwa kwa Hazrat Nabii Yusuf Msema kweli (AS), alikiwaalika (alikiwalingania) na kuwapa wito wa kuelekea kwenye imani ya Mungu Mmoja (Tauhidi) na kumwabudu Mungu Mmoja.

Utaratibu huu uliendelea kwa namna ambayo hata Maofisa (wa jela) waliokuwa wakimchunga walishtuka kwa kuona hali ya mtu huyu nao wakawa watu wa ibada.

Serikali ilipoona kwamba haiwezi kuwateua maafisa waislamu ili kumchunga, iliamua kuwateua maafisa wawili wa Kiyahudi (ili kumchunga).

Lakini hatimaye wakawa Waislamu kwa muda mfupi tu, kisha wakajifunza hukumu za Kiislamu na kuanza kuabudu (kufanya ibada).

Kisha wakateua maofisa wawili wa Kikristo wa (kumtunza na) kumchunga, nao wakawa Waislamu.

Alikuwa na imani yenye nguvu na amali safi (za ikhlasu) kiasi kwamba upendo wake ulikuwa moyoni mwa kila mtu.

Maswahiba wa Alim (Mwanazuoni) huyu mkubwa bila kukusudia walijikuta wanakuja kwenye upande wa Dini safi ya Uislamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha