Thursday 23 January 2025 - 14:21
Mahali pa kuuawa Kishahidi kwa Syed Nasrullah ni Qiblah ya watu huru wa ulimwengu na watu wa Upinzani (Muqawamah)

Ujumbe wa vuguvugu la "Al-Nasr Amal", linaloongozwa na Malhem Al-Hujairi, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Lebanon, ulitembelea mahali alipouawa Shahid Syed Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon.

Kulingana na kikundi cha Tarjama cha wakala wa Habari wa "Hawzat", Ujumbe kutoka vuguvugu la "Al-Nasr Amal", ukiongozwa na Melhem Al-Hujairi, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi la Lebanon, ulitembelea mahali alipouawa Shahidi Syed Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon katika eneo la "Hare Harik" la Beirut na kuweka maua eneo hilo na kwa roho ya Shahidi huyu na roho za Mashahidi wa Upinzani (Muqawamah) na Mashahidi wa Taifa hilo, na ukawasomea Suratul Fa'tiha.

Katika Hotuba yake Al-Hajiri, Mwakilishi wa Wananchi alisisitiza juu ya kushikamana na Upinzani / Muqawamah na kutokata tamaa hadi malengo ya Taifa ya Uhuru, Utu na Ukombozi wa Taifa yatimie.

Alibainisha akisema: Mahali hapa patakatifu patakupa hisia ya heshima ambayo imechanganyikana na huzuni ya kuwapoteza Mashahidi hao; na hadhi, utu na (adhama) ukuu.

Mwakilishi wa Bunge la Lebanon akaendelea kusema:

Hapa ni sehemu ambayo Shahid mkubwa na wa ngazi ya juu na Bwana wa Mashahidi wa Ummah, Syed Hassan Nasrullah aliuawa Shahid, hapa ni mahali kilipo Kibla cha watu huru wa Dunia, watu watukufu, Wapiganaji na watu wa Upinzani / Muqawamah, ili kitupe (kibla hicho) roho ya uamuzi, nguvu na uthabiti ndani yetu.

Mwishowe, alisema: Leo, wakati Gaza imewashinda wauaji, wahalifu na wavamizi, tumekuja kufanya upya agano na uaminifu katika mstari na njia ambayo Shahid wetu Mtukufu Syed Hassan Nasrullah aliuawa Shahid ndani yake, na kuhifadhi Umoja wa Taifa; na hatimaye tushikamane na kanuni na misimamo ya kitaifa na suala letu kuu, ambalo ni Palestina, na tuhifadhi Upinzani (Muqawamah) kwa macho yetu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha