Kulingana na kundi la Tarjama la Shirika la Habari la Hawza, Urusi ni nchi kubwa yenye idadi ya watu milioni 146, na Waislamu wapatao milioni 25 wanaishi katika nchi hii.
Urusi ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu katika upande wa (Bara la) Ulaya. Watu wengi nchini Urusi wanafuata Ukristo wa Orthodox.
Katika nchi hii, nyakati za kufunga wakati mwingine hufikia saa 22, jambo ambalo limeifanya nchi hii kuwa miongoni mwa nchi zenye mfungo mrefu zaidi duniani.
Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, tofauti na nchi nyingi za Kiislamu ambazo hubadilisha saa zao za kazi au nyakati za likizo, Waislamu wa Urusi huendeleza maisha yao ya kila siku kama kawaida.
Mojawapo ya Desturi / Mila za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani nchini Urusi ni kufanya (kuandaa) futari ya watu wengi, ambapo Wasomaji wa Qur'an na Wataalamu wa Kiislamu hualikwa (katika mkusanyiko huo futari).
Your Comment