Kulingana na Mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, katika hafla iliyohudhuriwa na wasomi na wataalam wa Sheria na masuala ya kiuchumi, na vile vile Mkurugenzi wa Seminari nchini (Iran) na Mkuu wa Benki Kuu, Mkusanyiko wa kazi / athari za "Sheria / Fiqh ya Soko la Hisa na Karatasi za Hisa" zilizinduliwa jioni ya Jumatatu, Februari 24, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Usimamizi cha Hawza Mjini Qom.
Katika hafla hii, ambayo ilifanyika kwa uwepo wa baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Seminari, Jumuiya ya walimu wa Seminari ya Qom, wawakilishi wa nyumba za Marajii Taqlid, wakuu wa Seminari na vituo vya Kisayansi vya Chuo Kikuu, Hojjat al-Islam wal-Muslimeen Ali Andalibi, Mwandishi wa Kitabu cha: "Fiqh ya Soko la Hisa na Karatasi za Hisa", alielezea umuhimu wa masuala ya kiuchumi katika Fiqh ya Kisasa, ambapo alisema: Kitabu hiki ni matokeo ya miaka kadhaa ya juhudi za Ofisi ya Fiqh ya Kisasa ya Seminari za Kielimu na usaidizi wa Maprofesa mashuhuri katika uwanja huu.
Ameongeza kuwa: Baada ya takriban miongo mitano kupita tangu Mapinduzi ya Kiislamu, pamoja na maendeleo ya miundombinu, ulazima wa kuendeleza na kuimarisha programu za kifiqhi na kisheria unahisiwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule. Ni muhimu kwamba maeneo haya ya programu, ikiwa ni pamoja na (Fiqh) Sheria za Kiuchumi, kujadiliwa kwa umakini na kuchunguzwa katika mazingira ya Seminari (Hawza).
Amezitaja changamoto za nyanja mbalimbali zikiwemo za kifamilia, kimaamuzi, kiuchumi na kiutamaduni kuwa ni masuala ya kimsingi ya jamii ya leo na kusisitiza: Masuala hayo yanapaswa kufanyiwa utafiti na kufundishwa mara kwa mara na Mafaqihi (Wanazuoni wa Sheria / Fiqh ya Kiislamu) na mada zinazohusiana na hayo zitungwe kwa utaratibu.
Your Comment