Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Hojjatul-Islam wal-Muslimeen Sayyid Hashim Al-Haidari, katika hotuba yake kwenye hafla ya mazishi ya Shahidi Sayyid Hassan Nasrallah na Sayyid Hashim Safiyyud-din katika Haram / Madhabahu Takatifu ya Bibi wa Karamat, akiashiria juu ya mazishi ya Sayyid Hassan Nasrallah, alisema: Alikuwa ni mtu Jasiri (Shujaa), Mwaminifu, Mkweli na Mwanajihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu na Mwanafunzi wa Shule ya Imamu na Wilayatul Faqih.
Akieleza kuwa Sayyid Hassan Nasrallah alisimama dhidi ya Israel kwa ujasiri kamili, kwa imani, kwa ikhlasi na utambuzi katika miaka hii, na alikuwa Katibu Mkuu wa Hezbollah ya Lebanon kwa muda wa miaka 32 na askari mwenye mapenzi na ikhlasi kwa Waliyyu Amri al-Muslimin (ambaye ni Mtu aliye na sifa za kusimamia mambo ya kijamii ya Waislamu na kudhibiti hatima zao), alisema: Hakukuwa na hofu wala kukata tamaa katika moyo wa Sayyid Hassan Nasrallah, moyo wa Sayyid Hassan ulikuwa umejaa ujasiri katika Jihad ya Kijeshi na pia katika Jihad ya Tabyin.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ahdullah ya Iraq akibainisha kuwa moyo wa Sayyid Hassan ulikuwa umejaa matumaini, amesema: Hezbollah ilianzishwa miaka mitatu baada ya Ushindi wa Mapinduzi (ya Kiislamu ya Iran) kupitia Fat'wa ya Imam, wakati wa vita vilivyowekwa na wanafiki na wahaini nchini Iran, Imam alitoa amri na Fat'wa ya kuanzishwa kwa Hezbollah kutokana na maono yake ya busara na makubwa, na siku hiyo hiyo, Wanazuoni wa Lebanon wakiwa katika idadi ndogo ya vijana walianza Muqawamah wa Kiislamu dhidi ya jeshi lenye nguvu zaidi la Israel kwa wakati huo katika eneo zima la kikanda.
Ikiwa tutataka kurudi nyuma kwa sababu ya Kamanda mmoja kuuliwa Kishahidi, ni makosa
Sayyid Hashim Al-Haydari amesisitiza kwamba leo hii ni lazima tutembee kwa matumaini na ujasiri na bila ya woga wala kukata tamaa, na akaongeza kuwa: Ni makosa kutaka kurudi nyuma kwa sababu ya kifo cha kishahidi cha kamanda mmoja. Kazi ya Sayyid Hassan ilikuwa ni kumtegemea Mwenyezi Mungu na kuamini Aya Tukufu inayosema:«إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ» / " Ikiwa Ninyi Mtamnusuru Mwnyezi Mungu basi nae atakunusuruni" (Surat Muhammad: Aya ya 7).
Sayyid Hassan alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Hezbollah miaka 10 baada ya kuasisiwa Hezbollah na baada ya kuuawa Shahidi Sayyid Abbas al-Musawi, huku akiwa kijana mwenye umri wa miaka 33 na moyo wake ukiwa umejaa imani na mapenzi makubwa kwa Imam na Wilayat Al-Faqih.
Alisema katika kipindi cha miaka 16 niliyokuwa naye, sikumuona mtu kama yeye katika imani, itikadi na utiifu kwa Wilayat Al-Faqih, na akasema: Njia ya Sayyid Hassan ilikuwa ni njia ya Waliyyul - Faqihi, na wosia wa Sayyid Hassan daima ulikuwa ni kusisitiza kufuata na kuwa na utiifu na mapenzi kwa Waliyyu Amr al-Muslimin, na upendo mkubwa wa Sayyid Hassan Nasrallah kwa Hazart Imam Khamenei.
Akitoa Khutba katika Haram / Madhabahu Tukufu ya Bibi wa Karamat alisisitiza kwamba hii haikuwa kauli mbiu bali alikuwa ni mtu wa Jihadi ya Tabyin, na aliongeza kwa kusema: 8 Januari, 2022, pale Imam Khamenei aliposema kwamba Jihad ya Tabyin ni jambo la wajibu wa haraka na wa uhakika, Sayyid Hassan Nasrallah kabli ya Hukumu hii ya Waliyyul-Faqih alikuwa tayari ashaanza kufanyia kazi suala (jukumu) hilo, na kila Usiku na Mchana wa A'shura, katikati ya ulimwengu wa Kiarabu, bila ya kuwa na woga wowote, wala Taqiyya, alikuwa akitoa Bai'a ya Kisharia, kiakili, kidini, na Kiitikadi kwa Wilayat Al-Faqih.
Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa Shahidi wa Wilayat al-Faqih na Shahidi wa njia ya Imam Khomeini
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ahdullah ya Iraq alisema: Katika Mhimili wa Muqawamah, kuna watu wengi ambao ni Wana Muqawamah na wapinga kiburi (na uistikbari) wa Marekani na Israel; Lakini hawathubutu kueleza (naa kuweka) waziwazi imani hii na kutoa (Bai'a) kiapo cha utii kwa Waliyyu Amr al-Muslimin; Baadhi yao wanamtazama Sayyid Hassan Nasrallah kama Mwana Muqawamah (Mpinzani na mpambanaji dhidi ya Uistikbari), Ndiyo, ni kweli kabisa kwamba yeye ndiye Bwana wa Upinzani (Muqawamah), lakini Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa pia ni Shahidi wa Wilayat al-Faqih na Shahidi wa njia ya Imam Khomeini.
Ameeleza kuwa ushujaa wa Sayyid Hassan katika Jihadi yaTabyin ulikuwa mkubwa zaidi kuliko ushujaa wake katika Jihadi ya Kijeshi, na akasema: "Kutoa heshima (sharafu) ni jambo gumu zaidi kuliko kujitoa muhanga (kutoa uhai wako). Baadhi ya Maulamaa wa ndani na nje ya Iran ni Wanamapinduzi na ni Wafuasi wa Wilayat, na wana picha ya Kiongozi (Hazrat Ali Khamenei) kwenye kuta za nyumba zao (na ofisi zao), lakini wanaogopa kupanda juu ya mimbari zao na kuzungumza juu ya Wilayat."
Wosia wa Sayyid Hassan ulikuwa wazi juu ya Wilayat al-Faqihi
Sayyid Hashim Al-Haydari alisisitiza: Wosia wa Sayyid Hassan ulikuwa wazi juu ya Wilayat al-Faqih, na ikiwa Wanazuoni na Maulama katika ulimwengu mzima wa Kiislamu, hasa katika anga (au nafasi) za mitandaoni na kwenye mimbari, watakuwa kama Sayyid Hassan Nasrallah, basi kwa hakika hali itabadilika.
Sayyid Hassan alisema huko Beirut, mbele ya kashfa na mashambulizi makali kutoka kwa ulimwengu wa Kiarabu na maadui wa dhahiri kwamba, ninajivunia kuwa Mwanachama / Mfuasi wa chama cha Wilayat al-Faqihi.
Akieleza kuwa wosia wa Sayyid Hassan ni kunyanyua jina la Imam Khomeini (RA) na Wilayat al-Faqih, alisema kuwa: Mimi nikiwa Mwanajeshi mdogo katika mstari wa wa mbele wa mapambano ya Muqawamah, napenda kusema kuwa sote tunajua na kutambua kwamba lengo la kwanza la Marekani na Israel halikuwa Gaza na Palestina na Sayyid Hassan Nasrallah; Badala yake, lengo lao kuu na la kwanza ni Wilayat al-Faqih, na leo hii tunatangaza wazi kwamba maisha yetu tunayatoa (dhabihu) fidia kwa Kiongozi (Sayyid Ali Khamenei).
Mstari Mwekundu wa Sayyid Hassan Nasrallah ulikuwa ni Wilayat al-Faqih na Jamhuri ya Kiislamu
Akitoa Khutba katika Haram / Madhabahu Tukufu ya Bibi wa Karamat alifafanua akisema: Mstari mwekundu wa Sayyid Hassan Nasrallah ulikuwa ni Wilayat Al-Faqiha na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Kwa sababu kama kungekuwa hakuna Jamhuri ya Kiislamu, leo hii kusingekuwa na Hezbollah, na Sayyid Hassan Nasrallah asingekuwa Katibu Mkuu wa Hezbollah, na kusingekuwa na Mstari wa Mbele wa Mapambano ya Muqawamah. Lengo la Marekani na Israel ni mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu na Wilayat Al-Faqih; Kwa hivyo, kutetea, kuunga mkono na kuelezea juu ya Wilayat al-Faqih ni jambo lenye lazima zaidi.
Akasema: Baada ya kuanza vita huko Yemen, nilikuwa katika khidma / utumishi wa Sayyid Hassan, na aliniambia kuwa Marekani ilimtumia ujumbe kwamba ukitaka pesa nyingi tutakupa, ukitaka Serikali ya Lebanon tutaikabidhi mikononi mwako, tutakufanya wewe kuwa Sayyid al-Arab (Bwana wa Waarabu) lakini kwa sharti moja tu nalo ni kwamba uachane (uondokane ) na Wilayat al-Faqih na Jamhuri ya Kiislamu. Lakini Sayyid Hassan Nasrallah aliwapa jawabu lile lile alilolitoa Bwana Mtume (s.a.w.w) kwa viongozi wa Maquraishi, kwamba mkiliweka Jua katika mkono wangu wa kulia na Mwezi katika mkono wangu wa kushoto, sitoiacha (sitoachana na) njia ya haki (na iliyo sawa) na sitosalimu amri.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ahdullah ya Iraq amesema, kuwa kwa mujibu wa ibara ya Shahidi Soleimani, Iran ni Haram na akasema: Iwapo unatafuta Nyumba ya Fatima, ninaamini na kuitikadia ya kwamba baada ya Ushindi wa Mapinduzi na kuasisiwa Serikali ya Kiislamu, Nyumba ya Fatima iko hapa (Iran), na hapa (Iran) ndio Haram yetu, na Sayyid Hassan Nasrallah alikuwa ni Mwanajeshi wa Muqawamah (Upinzani) na Wilayat na Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu.
Upanga wa Sayyid Ali na Damu ya Sayyid Hassan kwa hakika vitashinda upanga wa Marekani na Israel
Sayyid Hashim Al-Haydari alibainisha: Katika maombolezo ya Sayyid Hassan Nasrallah, kulia tu hakutoshi; Bali tunapaswa kumfuata Sayyid Hassan Nasrallah kwa kufanya Jihadi ya Tabyin, na tujue kwamba upanga wa Sayyid Ali na Damu ya Sayyid Hassan Nasrallah, kwa hakika vitaushinda upanga wa Marekani na Israel.
Your Comment