Sunday 23 February 2025 - 12:55
Seminari inasimama katika ahadi yake kwa Upinzani (Muqawamah) wa kujivunia / «إنّا علی العهد»"Hakika sisi tupo katika Ahadi" ni kauli mbiu ya siku zote ya Waseminari (Wana Hawza)

Mkurugenzi wa Seminari zote nchini (Iran) amesisitiza kwamba ujumbe wa Seminari (Hawza) ya Faiziyah na Mji wa Qom kwa Muqawamah (Upinzani) na mazishi ya Sayyed wa Muqawamah (Upinzani) ni huu kwamba wanaseminari (Wana Hawza) watabaki kuegemea kwenye maagano (ahadi) yao na Mwenyezi Mungu katika mafundisho, mahubiri na juhudi (ijtihada) zao, na akasema: Seminari (Hawza) inasimama katika ahadi yake ya zaidi ya miaka 60 ikiwa pamoja na Imam wa Mashahidi, Uislamu Mtukufu, Mapinduzi na Nidhamu (Mfumo wa Serikali) ya Kiislamu, Upinzani (Muqawamah) wa Kiislamu, na mfumo wa Wilayat Al-Faqih.

Kwa mujibu wa ripota wa Shirika la Habari la Hawza, Mkurugenzi wa Seminari zote nchini (Iran) katika kikao chake cha kirafiki (na ukaribu) na Maprofesa na Wanafunzi wa Seminari (Hawza), alitangaza kauli mbiu ya Seminari hizo katika mkesha wa kuzikwa Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah kuwa ni «إنّا علی العهد»"Hakika sisi tupo katika Ahadi" na akasema: "Kauli mbiu yetu sote ni kwamba tunasimama juu ya Ahadi ya Upinzani (Muqawamah) na mazungumzo ya Mapinduzi ya Kiislamu." Huu ni ujumbe wa Seminari za Fayziyah na Dar al-Shafa kwa watu wote waheshimiwa wa Upinzani (Muqawamah) na Hezbollah.

Mkurugenzi wa Seminari alisema: Wote wenye kibri (Uistikbari) katika Ulimwengu na watu wote wenye nia mbaya wa ndani na nje ya nchi, wasiwe na shaka yoyote kwamba Seminari (Hawza) ya Qom, kwa neema ya Mwenyezi Mungu, ilikuwa, na iko, na itaendelea kuwa Seminari yenye nguvu na imara (kama chuma).

Mkurugenzi wa Seminari alisema kwamba Wanafunzi wote wa Seminari (Hawza) walikuwa na shauku ya kuwa katika msafara wa mazishi ya Kiongozi wa Upinzani (Muqawamah) Sayyid Hassan Nasrullah, na kwa sababu ya kunyimwa (na kukosa) neema ya uwepo huu, wanahisi mzigo mkubwa sana kupindukia, na akasema: Mara nyingi nilitumia muda mwingi huko Dahiya kuanzia usiku hadi asubuhi nikiwa pamoja na Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah na ninakumbuka matukio mengi na masomo mengi matamu (na mazuri) yenye kufundisha kutoka kwake.

Ayatollah Arafi alimchukulia Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah kuwa ni mtu mjuzi, shujaa, mwenye hekima, mwenye mwamko, mwenye maono (utambuzi), mwenye utulivu, mwenye tabia njema, mvuto na ushawishi mkubwa, ambaye alibadilisha milingano ya eneo la kikanda kwa kuzingatia fikra za Imam Khomeini (RA) na mazungumzo ya Mapinduzi ya Kiislamu na uongozi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sayyid Ali Khamenei).

Huku akiashiria kwamba hivi leo Ulimwengu umehamasishwa na Kiongozi wa Muqawamah dhidi ya dhulma, uistikbari na ukandamizaji, Mkurugenzi wa Seminari nchini (Iran) ameongeza kwa kusema kuwa: Wajue (hao maadui ya) kwamba mapigo yanatufanya tuwe imara na Upinzani (Muqawmah) zaidi na kwamba Hezbollah, Hamas na Muhimili wa Muqawamah wataendelea (na kusonga mbele) katika njia yao kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, na azma na nia hii itadhihirika katika maonyesho makubwa ya Beirut.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha