Sunday 16 February 2025 - 19:01
Kufukuzwa kwa raia 700 wa Pakistan wa Bahrain kwa kuwa Shia

Serikali ya Bahrain hivi majuzi iliwafukuza Wapakistan 700 ambao hapo awali walipewa uraia. Watu hawa ambao waliajiriwa zaidi kama vikosi vya usalama, wamepigwa marufuku kuendelea kukaa Bahrain kutokana na kushikamana na Madhehebu ya Shia.

Kwa mujibu wa kundi la Tarjama la Shirika la Habari la Hawza, tovuti ya “Mir’at” – Mirror – ya Bahrain iliandika: Katika ukaguzi wa sera za kutoa uraia wa Bahrain, ushahidi mpya unaonyesha kuwa Serikali ya nchi hii imewatimua baadhi ya watu ambao iliwapa uraia katika miaka ya nyuma.

Kwa mujibu wa ripoti, ili kubadilisha muundo wa idadi ya watu na kuimarisha misingi yake ya madaraka, serikali ya Bahrain katika miaka ya nyuma iliwapa uraia raia wa kigeni, na katika suala hili, imetoa kipaumbele kwa kufutwa uraia kwa watu ambao wanaonyesha kuwa wafuasi wa Madhehebu ya Shia.

Hapa suala la kuwapa Wapakistan uraia wa Bahrain linaibuliwa. Kwa mujibu wa habari za hivi punde, Serikali ya Bahrain imewafukuza Wapakistan 700 ambao hapo awali iliwapa uraia. Sababu ya hili ni utegemezi (na ufuasi) wa watu hao kwenye Madhehebu ya Shia, jambo ambalo haliendani na mipango ya serikali ya kubadilisha muundo wa idadi ya watu nchini.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha