Tuesday 11 February 2025 - 12:54
Nafasi ya Mtandao; Ni sehemu mpya ya maisha au ni tishio kwa utambulisho wa Mwanadamu wa Kisasa?

Hojjatul-Islam wal-Muslimin Barteh alisema: Ikiwa hatuelewi nafasi ya mtandaoni kwa usahihi, basi tunaweza kupoteza utambulisho wetu na maadili katika bahari isiyo na mwisho wa habari.

Kulingana na Shirika la Habari la Hawza, katika Ulimwengu ambamo mtandao unabadilisha kwa kasi mitindo ya maisha na maadili ya kibinadamu, tablighi (propaganda) na mawasiliano pia yamechukua sura mpya. Katika mahojiano na Shirika la Habari la Hawza, Hojatul-Islam Barteh alifanya uhakiki na uchunguzi juu ya athari kubwa za anga za juu kwenye tabia na mawazo ya wanadamu wa kisasa na akaonya: "Ikiwa hatutaelewa nafasi hii ya mtandao kwa usahihi, basi tunaweza kupoteza utambulisho wetu na maadili katika bahari hii isiyo na mwisho wa habari."

Katika mahojiano na Shirika la Habari la Hawza, Hojjatul Islam Barteh alijadili tofauti kati ya tabligh mtandaoni na tabligh ya ana kwa ana na kusisitiza: Uelewa sahihi wa anga ya mtandaoni ni hatua ya kwanza ya matumizi bora ya uwanja huu.

Kulingana na yeye, mwanadamu wa sasa, kwa sababu ya kuathiriwa na kushawishiwa na (nafasi au) uwanja wa mtandao, amehama kutoka kwenye tabia ya maneno na vitendo hadi kwenye tabia ya kuona, na mabadiliko haya yameunda maadili mapya.

Profesa wa Hawza na Chuo Kikuu alisema kuwa katika (uwanja au) nafasi ya mtandao, kuonekana na kujulikana (kuwa mashuhuri) limekuwa ni jambo la thamani. Badala ya maadili kama vile kujitahidi (kufanya ijitihada) na unyenyekevu, umaarufu na kujionyesha vinapewa kipaumbele zaidi leo hii (katika mitandao ya kijamii). Watu wengine wako tayari hata kufanya mambo machafu au ya kufedhehesha ili mradi waonekane. Mabadiliko haya ya maadili yanaonyesha athari kubwa ya nafasi ya mtandao kwenye tamaduni na utambulisho wa kisasa wa Binadamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha