Tuesday 11 February 2025 - 10:38
Kituo cha Majini cha Bangladesh kimepewa jina la Mwanachuoni huyu wa Kishia

Haji Mohammad Mohsen, Mwanzilishi wa Shule za Kidini huko Bangal Magharibi na Bangladesh, alikuwa na athari kubwa kwa jamii kwa kukuza maarifa ya kidini na wakfu za kielimu.

Kulingana na Shirika la Habari la Hawza, Haji Mohammad Mohsen Khair, maarufu katika historia ya Bara (au Kontinenti) ndogo, alizaliwa Januari 3, 1732 huko Hooghly, Bengal Magharibi, India.

Jina lake daima hutajwa kama mfano hai wa ukarimu. Hii ni kheri kubwa inayoheshimiwa na watu wote wa Bengal, sawa sawa wawe ni Waislamu au Wahindu.

Mmiliki wa mali nyingi na roho kubwa

Haji Mohammad Mohsen alikuwa mmiliki wa mali kubwa ambayo aliitoa kwa ukarimu (wake). Baba yake, Haji Faizullah, ambaye alikuja Bengal kutoka Iran, alikuwa mmiliki mkubwa wa ardhi na tajiri. Mama yake Zainab Khanum pia alikuwa na ardhi kubwa huko Hooghly, Jeshur, Murshidabad na Nadia.

Baada ya kifo cha dada yake Mannojan, Haji alirithi mali yake. Hata hivyo, alikuwa mtu wa kidini sana na asiye na majivuno na kibri, na alichagua kuishi maisha rahisi.

Hakuishi katika kasri alilojenga, bali alikaa kwenye kibanda kidogo karibu na kasri la Imambareh.

Alipata pesa kutokana na kunakili (au kutoa nakala / kopi za) Qur’an na akatumia pesa hizo hizo kuishi maisha yake. Alikuwa anapika chakula chake kwa mikono yake mwenyewe na anakula na wasaidizi wake.

Haji Mohammad Mohsen alianza elimu yake ya awali chini ya usimamizi wa Mwalimu binafsi na kisha akaenda Mji Mkuu wa Murshidabad kuendelea na elimu yake. Baada ya kumaliza masomo yake, alisafiri kwa muda wa miaka 27 na kuzuru Makkah, Madina, al-Kufa, Karbala, Iran, Iraq, Arabia na Uturuki kisha akarejea nchini kwake.

Kwa kutumia utajiri wake, alianzisha taasisi nyingi za elimu. Zifuatazo ni wakfu zake za kielimu: "Chuo Kikuu cha Mohsen Hooghly", "Chuo cha Serikali cha Haji Mohammad Mohsen Chittagong" na "Shule ya Sekondari ya Dolatpour Mohsen", ambavyo ni vyuo vya kielimu vilivyoanzishwa.

Msaada wake katika baa la njaa na uanzishwaji wa Mfuko wa Mohsen

Wakati wa baa la njaa la mwaka 1769 - 70, Haji Mohsen alianzisha vituo vingi vya misaada na kuchangia mfuko wa Serikali. Mnamo 1806, alianzisha mfuko ulioitwa "Mohsen Fund" ambao ulijitolea kwa ajili ya shughuli za kidini, (masuala la) kustaafu, masomo na hisani.

Mfadhili huyu wa kidini alikufa huko Hooghly mnamo 1812 na akazikwa huko Hooghly Imambareh.

Jina la Haji Mohammad Mohsen ni la milele katika historia kwa anuani ya mfadhili mkuu. Katika kumuenzi na kuhuisha kumbukumbu yake, Ukumbi wa Mohsen wa Chuo Kikuu cha Dhaka (Bangladesh) uliitwa kwa jina lake.

Pia, Mfuko wa Mohsen mpaka leo bado unaendelea kusaidia elimu ya wanafunzi wenye uhitaji na maskini. Kituo cha Kijeshi cha Wanamaji cha Bangladesh huko Dhaka pia kimepewa jina lake na kinajululikana kama: Haji Mohsen Naval Base (Kambi ya Wanamaji ya Haji Mohsen).

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha