Monday 10 February 2025 - 17:37
Vyombo vya Habari vya Saudia vimemkosoa vikali Netanyahu

Katika hali ya kuongezeka kwa mvutano kati ya Saudi Arabia na Israel, Kanali ya Televisheni ya Saudia ilimshambulia Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu. Shambulio hili lilitokea baada ya taarifa za hivi majuzi za Netanyahu kuhusu pendekezo la kuunda Taifa la Palestina nchini Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa kundi la Tafsiri la Shirika la Habari la "Hawza", Tovuti ya Kielektroniki ya Russia Today (RT) iliandika: Katika ripoti ya hivi karibuni ya Kanali ya Habari ya "Al-Akhbariyya" ya Saudia, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel alikosolewa vikali.

Mtandao huu ulimtaja na kumsifu kuwa yeye ni mtu mwenye sura moja ya uvamizi (na ukaliaji kwa mabavu) na kusisitiza kuwa uavamizi (na ukaliaji wa nchi za wengine kwa mabavu) kamwe hauna sura mbili: Sura nzuri na nyingine sura mbaya, bali sura yake ni moja tu, na sura hiyo moja na mbaya ni Netanyahu. Ripoti hii ilichunguza historia ya familia ya Netanyahu na sera yake kali na kumwita "Mzayuni Mwana wa Kizayuni".

Kulingana na ripoti hii, Netanyahu alirithi misimamo mikali kutoka kwa familia yake. Babu yake alikuwa rabi mwenye msimamo mkali na baba yake alikuwa mwandishi wa Kizayuni mwenye mielekeo mikali.

Mtandao huo pia ulibainisha kuwa Netanyahu anajiona kuwa ni "zawadi kutoka kwa Mungu" na hata kubadili jina lake kuwa "Netanyahu" ambalo linamaanisha "Zawadi kutoka kwa Mungu". Hii inaonyesha aina ya kujiona ambayo imepitishwa kwake kutoka kwa familia yake.

Al-Ikhbariyya iliongeza: Netanyahu ametumia ghasia ambazo hazijawahi kutokea kwa miongo mitatu na hana ufahamu wa amani. Anachokijua tu ni lugha ya vurugu na kutumia zana za kijeshi, na anakataa suluhisho lolote lile la amani.

Ukosoaji huu mkali wa vyombo vya habari unaibuliwa katika hali ambayo mivutano kati ya Saudi Arabia na Israel imeongezeka kutokana na matamshi ya hivi karibuni ya Netanyahu kuhusu pendekezo la kuachia sehemu ya ardhi ya Saudia kwa ajili ya kuasisiwa Taifa la Palestina.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha